» » Unajua Namna Ya Kutafuta Simu Iliyopotea?

 Njia hii inatumika endapo simu yako haikubadilishwa laini na haikuzimwa data, na mara nyingi tunatumia njia hii kutafuta simu zilizopotelea mazingira ya karibu na tunapoishi.
Ok, Kila mtu anaetumia Smartphone (hasa android base smartphones) anafahamu wazi kuwa mwanzoni kabisa unatakiwa kujaza kitu kinaitwa Gmail Account pamoja napassword zako.
Wengi wetu hupuuza hii Gmail Account pengine huwa tunawapa mamlaka watu wengine kutujazia bila hata kuulizapassword walizotuwekea, hivyo basi ninakushauri kufanya uwezavyo kukariri Gmail Account yako iliyotumika kwenye simu yako pamoja na Password zake.
Sasa tuchukulie ulikuwa una simu yako, pengine ulikuwa na watu unaowafahamu, wakakuibia au wakaamua kukufichia,
Hatua ya kwanza kubwa unayotakiwa kufanya, baada tu ya kugundua umeibiwa, hapohapo omba simu ya mtu mwingine haraka iwezekanavyo au kimbia internet cafe kwenye Computer yenye mtandao (kabla hata huyo mwizi au aliyekufichia hajazima simu au data)
Ukipata simu au Computer iliyoungwa mtandaoni, basi fungua kiingilio cha google/internet/browser yoyote unayoweza kuingilia google, inaweza kuwa Mozilla, Chrome au Opera.
Fuata hatua zifuatazo kuitafuta simu yako;
  1. Ikifunguka itakuja hivi,

  2. Max IT Club Android Lost 1Kisha unatakiwa kuandika maneno haya (gmail) hapo kwenye sehemu ya kuandikia, na baada tu ya kuandika utaona imetokea kama picha hii inavyo onyesha,

  3. Max IT Club Android Lost 2Unachotakiwa kufanya ni kubonyeza hicho cha kwanza kabisa kilichoandikwa (Gmail – Google), na baada tu ya kukibonyeza utapelekwa sehemu hii kama picha inavyoonyesha hapa chini,

  4. Max IT Club Android Lost 3Ninaamini kuwa ukiangalia hapo kwenye picha namba 3 unaona sehemu imeandikwa “Enter your Email“, basi hapo unatakiwa uandike “Email yako ambayo ulikuwa unaitumia kwenye hiyo smartphone iliyopotea/kufichwa”

  5. Pia ifahamike kama umeomba simu ya mtu, pengine unaweza kukuta amesign in automatiki kwenye Gmail Account yake, kwa hiyo inabidi asign out kwanza ili uweze kuingiza “Gmail Account yako”

  6. Sasa basi tuendelee, ukishajaza Email yako hapo, unatakiwa kubonyeza “Next“, na itakupeleka sehemu nyingine ya kujazaPassword kama picha hii hapa chini inavyoonyesha,

  7. Max IT Club Android Lost 4Ukiangalia vizuri utaona sehemu imeandikwa “Password“, hivyo basi unatakiwa ujaze Password za Account yako ya Gmail uliyoweka kwenye simu yako iliyopotea au kufichwa, na baada ya kujaza Password piga tiki kabisa hapo palipoandikwa “Stay signed in” kisha bonyeza hilo neno “Sign in“, itakupeleka ndani ya Account yako ya Gmail kama picha hii hapa chini inavyoonyeha,

  8. Max IT Club Android Lost 5Sasa basi ikiisha funguka hivyo unatakiwa kurudi mwanzo kabisa yaani kule kwenye Google ambako ni pakutafutia vitu, na ukifika huko andika maneno haya “android/device manager” kisha bonyeza sehemu ya kusearch utaona vitu vimetokea kama picha hii hapa chini inavyoonyesha,

  9. Max IT Club Android Lost 6Sasa basi baada ya kutokea hicho kitu unatakiwa kubonyeza hapo nilipopawekea box, na ninaamini una macho mazuri kuona pameandikwa vipi (Android Device Manager – Google), na baada tu ya kupabonyeza utapelekwa moja kwa moja kwenye page ya kutafuta simu yako, angalia vizuri page hiyo inavyoonekana kwa kutazama picha hii hapa chini,

  10. Max IT Club Android Lost 7Sasa basi hapo nitakueleza namna ambavyo tunatumia hii sehemu,

  11. Kwanza kabisa ukiangalia hiyo picha ktk namba tisa hapo juu utaona kuna maneno kama, “Vodafone Smart…“, neno lingine ni “Connecting Your Device“, kuna maneno mengine kama “Ring“, “Lock“, na “Erase“, sasa ili nikurahisishie na ili uweze kunielewa vizuri tazama picha hii hapa chini,

  12. Max IT Club Android Lost 8Ninaamini hapa umekiona ninachokimaanisha, sasa basi nitaanza kuelezea kimoja baada ya kingine,

  13. Tukianza na hilo neno “Vodafone Smart…“, hapo ndipo litatokea jina la simu yako, huo ni mfano tu na hilo ndio jina la simu yangu mimi japo halikumalizia neno la mwisho, hivyo basi ukifanikiwa kufika hapo utaweza kuona jina la simu yako ambayo ilijazwa Email na Password zako na ndizo hizo ambazo leo tumezitumia kuingia kwenye Email yako kupitia simu ya mtu mwingine au Computer. (kama haujaelewa vizuri basi kamata neno moja tu kuwa hapo ndipo linakaa jina la simu yako)

  14. Utaona nimetumia box la njano kuonyesha maneno “Connecting Your Device“, hapo maana yake simu ya mtu mwingine uliyotumia au Computer inajiunganisha na simu yako iliyopotea au kufichwa, na ikimaliza tu itakuonyesha ipo wapi na tarehe ya mwisho kuwashwa data, na kama ipo online itakuonyesha hapahapo.

  15. Ukiangalia vizuri ktk picha hiyo utaona kuna namba moja ina mshale unaoonyesha neno Ring, maana yake unaweza kubonyeza hapo na ukailiza simu yako kwa lazima na kwa muda wa dakika tano na hata kama sauti imepunguzwa hadi mwisho, yenyewe italia kwa sauti kubwa ya mwisho ya simu yako na hapo hapo kama ipo karibu utaipata au kumkamata aliyeiba au kuficha. (Angalizo ujuzi huu utafanya kazi endapo aliyeiba au kuficha amewasha data ya simu yako na hakubadilisha laini yako, na ndio maana tunasema zoezi hili linapaswa kufanyika pale tu umegudua umeibiwa au kupoteza simu yako na lifanyike kwa haraka sana)

  16. Ukiangalia vizuri utaona kuna namba mbili hapo ina mshale unaoelekea kwenye neno “Lock“, maana yake ukibonyeza neno “Lock” utaifunga simu yako na huyo aliyeiba au kuficha hatoweza kuitumia labda akaflash, hivyo basi hii ndio option bora endapo zimepita siku chache halafu ukaja kuibahatisha siku moja ipo hewani, basi ifunge loki kwanza halafu endelea kuitafuta, (Angalizo ujuzi huu utafanya kazi endapo aliyeiba au kuficha amewasha data ya simu yako na hakubadilisha laini yako, na ndio maana tunasema zoezi hili linapaswa kufanyika pale tu umegudua umeibiwa au kupoteza simu yako na lifanyike kwa haraka sana)

  17. Ukiangalia kwa mara nyingine hapo utaona namba tatu hapo ina mshale unaonyesha neno “Erase“, maana yake ukibonyeza hilo neno utafuta kila kitu kilichokuwa kwenye simu yako, na huyo aliyeficha au kuiba hatokuta kitu chako tena, (Angalizo ujuzi huu utafanya kazi endapo aliyeiba au kuficha amewasha data ya simu yako na hakubadilisha laini yako, na ndio maana tunasema zoezi hili linapaswa kufanyika pale tu umegudua umeibiwa au kupoteza simu yako na lifanyike kwa haraka sana)

  18. Kumbuka, bila kusign in kwa Gmail Account yako kwanza, hautaweza kufanya kitu chochote

  19. Ninaomba kutoa wito kwa wale wazembe kuanza kuzifahamu email zao pamoja na password zako sababu teknolojia inakua kwa haraka, sana kuna mambo mengi mazuri yanakuja mtashindwa kuyapata kwa sababu ndogo ndogo zisizo za msingi

  20. Na mwisho kabisa ninaomba nikueleze kitu kimoja cha muhimu, ninafahamu wazi kuwa unawaza ni njia ipi utatumia kuipata simu yako endapo laini imetolewa na data imezimwa, ok usihangaike, endelea kutembelea site yangu ipo siku nitakuwekea posti hiyo.
Karibu sana.

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply