» » Jifunze jinsi ya kuweka Drivers zinazo kosekana katika Computer Yako

Kuna njia kuu tatu za kuweka/kuinstall drivers ktk Computer, nazo ni;
  1. Kwa kutumia CD au DVD
  2. Kwa kutumia flashi au external hard disk
  3. Kwa kutumia software maalum zifanyazo kazi na mtandao
1. Kutumia Cd/Dvd
Hapa ni lazima drivers ziwe zimechomwa/burned kwenye Cd au Dvd, mara nyingi watu hupenda kutumia “Driver Park Solution”, Hii ni aina fulani ya software inayokuwa ktk mfumo wa folder moja ambalo lina driver za kila aina ya computer. Saizi ya Folder lenye software hii ni kubwa sana almost GB 12, hivyo sio rahisi kukutumia kwa mtandao, tunaweza tuma DVD yake kwa njia ya basi endapo mtu anahitaji. Licha ya kuwa software hii huonekana kama imekamilika, lakini kuna baadhi ya computer huwa hazikubali baadhi ya drivers na zinataka uweke moja kwa moja kutoka mtandaoni.
2.  Kutumia Flashi au external hard disk
Njia hii haina utofauti na ile ya kwanza kwani hapa, ni lazima drivers ziwe zimekopiwa ktk flash au external hard disk, mara nyingi watu hupenda kuweka software hii ( “Driver Park Solution” ) ktk externa au flash sababu vinarahisisha uwekaji wa drivers ktk computer kwani ni vifaa vyenye spidi zaidi kuliko CD au DVD.
3.  Kutumia software zifanyazo kazi na mtandao
Njia hii ina utofauti mkubwa na hizo mbili za kwanza. Hapa mara nyingi kama kuna driver inakosekana basi jambo la kwanza kufanya nikuhakikisha Computer yako imeunganishwa na mtandao/yaani internet. Unaweza unganisha kwa kutumia njia tatu ambazo ni rahisi tu, nazo ni;
  1. Kwa kutumia modem
  2. Kwa kutumia simu yako kwa maana ya wireless hotspot
  3. Kwa kutumia simu yako kwa maana ya tethering hotspot (tumia USB Cable)
Baada ya hapo;
  1. Hatua yakwanza nikudownload folda letu lenye hizo software kupitia link niliyotoa hapo chini
  2. Ukimaliza kudownload hilo folder, utaliona ktk mfumo wa zipped folder
  3. Basi lifungue na ndani utakuta software mbili zikiwa na majina ya “driver easy” na “slim drivers”
  4. Kama kawaida utaanza kuinstall kwa kudouble click, zikihitaji password wakati wakuinstall tumia “maxitclub” bila alama za fungua na funga semi
  5. Install software mojawapo kati ya hizo
  6. Kisha itadownload baadhi ya vitu vyake kutoka mtandaoni kwa muda wa sekunde chache
  7. Fuata tu maelekezo mpaka utakapobofya button ya “finish”
  8. Kisha nenda ktk desktop kaifungue, utaona kunasehemu imeandikwa “scan”
  9. Maana ya hilo neno ni kwamba “scan computer yako moja kwa moja ikiwa mtandaoni ili uweze kuona drivers gani zinamiss
  10. Baada ya kuscan utaona kulia kumeandikwa maneno haya “update au download”
  11. Kwa atakaetumia “driver easy” ataclick download button kwa juu kisha ataona drivers zote zinazomiss
  12. Na kila driver ataona ina button yakudownload au updatekwa pembeni kulia
  13. Kwa ataae tumia “slim driver” ataona button imeandikwa “update” kwa pembeni kulia
  14. Basi wewe download kisha zikimaliza utakuwa unaona sehemu zimeandikwa “install”
  15. Endelea mpaka umalize, zingine huwa zinaomba uwe unarestart computer kila baada ya kuinstall driver moja, basi unachotakiwa kufanya nikurestart tu
  16. Kwa atakaetumia driver easy huwa inatoa option mbili za kuinstall yaani “auto” au “manual”, hapa unapaswa utumie manual huwa inakuwa option ya chini, ambapo utatakiwa kuipiga tiki kisha itakupeleka ktk folder linalosave drivers baada ya kudownload
  17. Na wisho endelea kufanya installation
  18. Kwa watakao tumia slim driver ni rahisi zaidi na sio complicated
Sasa download software hii kupitia link hii hapa chini;

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply