Hakika Huu ndio umekua mwaka wa mabadiliko makubwa kwa mtandao wa Instagram ukilinganisha na miaka mingine iliyopita.
Kumbuka mwaka huuu vitu kama logo, stories, kukuza picha, matangazo n.k vilianzishwa katika mtandao huu ili kuhakikisha tuu watu wanaufurahia zaidi na zaidi.
Sasa baada tuu ya kuongeza kipengele cha notification ambazo zinaonyesha picha, Instagram imeweka wazi kipengele kingine ambacho kinamruhusu mtumiaji wa mtandao huo kuweza ku’like comment au kuizima na vile vile hata kuwaondoa followers.
Hili watalifaidi wale ambao wata"update vifaa vyao vya iOs au Android kwenda katika toleo jipya zaidi.
Watumiaji watakuwa na uwezo wa kuweza ku’like comment za watu. Kama comment ikikurufahisha na hujisikii kuijibu au uko bize kidogo na majukumua unaweza ukagonga like tuu na mambo menginr yakaendelea. Kitu ambacho utatakiwa kufanya ni kobofya mara mbili (Kama wakati una like picha) katika kile kialama cha moyo pembeni ya comment ya mtu.
No comments: