Mtu mmoja kati ya watatu nchini Uingereza amegombana na mwenzake kuhusu utumizi wa simu kupitia kiasi kulingana na utafiti uliofanywa na Deloitte.
Mgogoro huo uliongezeka miongoni mwa watu wazima wenye umri wa kati ya miaka 25-34 kulinga na ripoti hiyo ,huku asilimia 11 ya watu wazima walio zaidi ya umri wa miaka 65 wakikiri migogoro kuhusu utumizi wa kupita kiasi wa simu.
Wanne kati ya watu watano nchini Uingereza wamenunua simu aina ya smartphone ,ikiwa ni sawa na watu milioni 37,Deloite imesema.
Watumiaji wa Smartphone sasa ni wengi zaidi ya wale wanaotumia laptopu.
Deloitte ilichunguza matumizi ya simu za takriban watu 4000.
Takriban watu 10 walikiri kutumia vipaza sauti vyao vya simu wakati wanapokula nyumbani ama katika mkahawa. Thuluthi moja walisema kuwa wanatumia simu mara kwa mara wakiwa na marafiki ama wakati wanapotazama runinga.
Smartphone huimarisha mawasiliano ,lakini matumizi yake kupitia kiasi huenda yakasababisha migogoro ,alisema Paul Lee mkuu wa teknolojia katika kampuni ya utafiti ya Deloitte.
No comments: