» » NJIA NYEPESI YA KUWEKA SLIDES KATIKA BLOG YAKO


Habari wapendwa leo nimeamua kuja na mada hii kutokana na sababu za msingi ikiwemo ya ongezeko la blogger wengi duniani kuongezeka kila siku. Watu wengi sasa wanamiliki blogu zaidi ya moja.Kama ni kweli basi somo hili litakusaidia kuongeza idadi ya watembeleaji katika blog yako.Kama una blogu zaidi ya moja basi blog moja weka hii widget katika blog yako.Usishangae hiyo widget ndio somo lenyewe tutakalojifunza.Hii itakusaidia kuongezeka kwa number ya page views katika blog yako. 



Kama nilivyosema mwanzo kwamba hii widget kwa ajili ya blogger itakusaidia kuonyesha kiautomatiki zile post zako na picha katika hizo post kwa mvuto unaomvutia msomaji. Hii widget hupokea mabadiliko yenyewe kiautomatiki pale unapotuma post mpya na hauhitaji ku edit widget, picha,kichwa cha habari wala maelezo tena. Unachotakiwa ni kuweka codi za widget hii katika blog yako na utakuwa umemaliza kazi.




Jinsi ya kuweka kodi za widget hii katika blog . 

Ili uweze kuweka fuata hatua hizi Nenda Blogger Dashbord→Add gadget→ HTML/Javascript. Baada ya hapo kopy kodi za hapa chini na uende ukazipaste hapo juu katika html/javascript.Ukisha paste kodi hizo bofya batani iliyoandikwa Save kisha malizia ku save mpangilio wa widget sehemu iliyoandikwa save arrangement. Ukimaliza ku save view blog yako na utaona hiyo widget inavyofanya kazi. 



Kodi zenyewe za kukopi hizi hapa. 

<link rel="stylesheet" type="text/css" href="http://blogger-json-experiment.googlecode.com/svn/resources/blogger-feed-rotator-plugin/default-style.min.css"/>
<div id="slider-rotator" class="slider-rotator loading"></div>
<script type="text/javascript" src="http://ajax.googleapis.com/ajax/libs/jquery/1.9.1/jquery.min.js"></script>
<script type="text/javascript" src="http://blogger-json-experiment.googlecode.com/svn/resources/blogger-feed-rotator-plugin/blogger-feed-rotator.min.js"></script>
<script type="text/javascript">
makeSlider({
url: "http://JINALABLOGYAKO.blogspot.com" // Add your blog URL
});
</script> 



Kumbuka kutoa jina la blogyako na kuandika jina halisi la blog yako. 

Ukiwa na tatizo toa maoni yako hapo chini. Siku njema wasomaji wangu tutaendelea kutoa mada tofautitofauti kupitia blog hii usisahau ku like page yetu ili upate habari zetu kwa urahisi.

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply