» » Kuangalia Chaneli Za Televisheni Za Tanzania Kwa Kutumia Simu Au Computer

Ni Kwa Mara Nyingine Tunakutana ktk Uwanja huu wa Teknolojia kwa lugha yetu.
Leo nimekuletea ujuzi juu ya namna ya kuangalia chaneli mbalimbali kwa kutumia Computer au Simu yako.
Nitaongelea Chaneli kwa pande Mbili tofauti;
  1. Chaneli za kwetu hapa Tanzania
  2. Chaneli za wenzetu nje ya Tanzania
Nikianza na Chaneli za Tanzania kama Azam Tv, Star Tv, ITV pamoja na TBC
Usipate tabu sana juu ya namna gani unaweza kuwa unaangalia Chaneli hizo nilizozitaja hapo juu na ili uweze basi unatakiwa kufuata hatua zifuatazo;
Naanza na watumiaji wa simu za Mkononi
  • Kwanza kabisa inabidi uwe na bando/au MB za kutosha
  • Kisha ingia ktk Play Store ya simu yako (Yaani kule huwa unachukulia Program/Applications Mbali Mbali
  • Kisha ukifika huko tafuta application program moja inaitwa“Puffin Web Browser”
  • Kwa hivyo unatakiwa uandike hayo maneno pale kwenye sehemu ya kutafutia kitu, na ukishaandika basi bonyeza “search” / “button ambayo mara nyingi huwa imechorwa alama ya lenzi”

    Max IT Club Puffin Screen Shot

  • Zitatokea nyingi sana, sasa basi ili kukusaidia nakuwekea picha yake hapa ili uichague kwa usahihi, na mara nyingi huwa inatokea ya kwanza kabisa baada ya kusearch
  • Picha yake ni hii hapa,

    Max IT Club Puffin Image

  • Baada ya kuipata sasa unaweza Kudownload na Kuinstall, na baada ya hapo, tunakwenda sasa kuangali hatua zitakazo tuwezesha kuangalia Chaneli Za Televisheni za kikwetu,
  • Ukimaliza tu kuinstall ifungue na utaona imefunguka kama ilivyo kwenye picha hii hapa chini,

    Max IT Club Puffin Appearance

  • Naamini ikifunguka hivyo basi utakuwa umeona hapo palipoandikwa “Search Keyword or URL”
  • Sasa basi ukiwa hapo hapo, Andika haya maandishi/link kama yalivyo na hakikisha haukosei hata kidogo,  Azam TV Live
  • Kisha bonyeza button ya kusearch/go ktk Keyboard Yako kama picha hii hapa chini inavyoonyesha,

    Max IT Club Azam Tv Live Search

  • Baada Ya Kusearch Utaona Matokeo Mengi sana, Unachopaswa kufanya Ni Kuchagu Tokeo la kwanza kabisa na kubonyeza hapo, kama picha hii hapa chini inavyoonyesha,

    Max IT Club Azam Tv Live Correct Sellection

  • Baada ya kubonyeza chaguo hilo la kwanza hakikisha imefunguka kama picha hii hapa chini inavyoonyesha,

    Max IT Club Clear View Of Tv Online

  • Kama ukiwa mdadisi mzuri basi ukiangalia hapo juu utaona button Ya ITV, TBC1, na Star Tv, Hivyo basi ukitaka kuangalia Chaneli nyingine unapaswa kubonyeza button yake.

Ninaomba kumaliza kipande hiki na watumiaji wa Computer
Ninyi ni watu wenye bahati sana, kwani hamuhitaji kuwa na “Puffin Web Browser” Bali mnachotakiwa kufanya ni kama ifuatavyo;
  1. Hakikisha una browser nzuri tu kama Mozilla Firefox au Chrome
  2. Hakikisha una adobe flash player ambayo ipo Up to date (Na hapa ninaweza kujibu swali kwa watumiaji wa simu kuwa kwanini tunatumia Puffin?, ni kwasababu haisumbui kwa maswala ya Flash players kama zilivyo browsers nyingine za simu)
  3. Kisha unganisha Computer yako ktk Mtandao
  4. Fungua Browser Yako na Search kama nilivyoelekeza hapo juu kwa kuandika Azam Tv Live
  5. Kisha chagua chaguo la kwanza kama nilivyoelekeza
  6. Baada ya hapo itafunguka kama ilivyofunguka ktk Simu
  7. Endelea na matumizi
Nakukaribisha sana ktk Uwanja huu wa ujuzi na juhudi za kwenda na wakati katika teknolojia.

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply