» » Epuka Kuibiwa Data Zako Muhimu Mitandaoni

Simu au Computer yako ina hizi tabia?

1. Kukuletea matangazo ya Kudownloada vitu usivyovijua?
2. kupokea emails nyingi za watu wanaomba account yako wakutumie hela?
3. kuletewa matangazo bila mpangilio wakati upo mtandaoni?
4. Kujiconnect kwenye website bila taarifa?
Kama unatatizo hata moja hapo, basi wewe ni muhanga wa hiki kitu ninachokieleza hapa chini;
Hii ni elimu muhimu kwako sababu itakuongezea usalama ktk mambo yako ya muhimu na siri zako unazotunza ktk mitandao kwa kutumia SIMU au COMPUTER yako.
Duniani kuna website za aina nyingi sana na zinafanya kazi kwa mifumo tofauti, na baadhi yetu hupenda kusafu mitandaoni kila siku kwa kutembelea website nyingi na kwa wingi.
Website hizo zinamilikiwa na watu tofauti na zipo kwa malengo tofauti na pia zinafanya kazi kwa mifumo tofauti,
Leo nitaongelea Website za aina fulani inayojulikana kwa jina la “Dark websites” yaani website giza au website nyeusi,
Sasa basi ninaomba niende moja kwa moja hapa kwenye mfumo unaotumika ktk hizi Dark Websites wakati wa utanyaji kazi;
Mara nyingi huwa zinaomba ujaze vitu vifuatavyo kabla haujaendelea na chochote;
1. Jina lako
2. Email yako
3. Password zako
Mfano mzuri ni kama (facebook, sasa basi naomba nieleweke kuwa kuna “Dark Website SALAMA” na pia kuna “Dark WebsiteHATARI“)
Licha ya kuwa Facebook ni aina ya “Dark website salama” lakini kuna watu walikwisha tengeneza website zinazofanana na facebook kwa kila kitu na hizo tunaziita “Dark websiteHATARI
Huo ni mfano mmoja tu, LAKINI zipo website za namna hiyo nyingi sana (Itafika siku nitakuonyesha ni namna gani Hackers huingilia Account za watu za Facebook) kwaleo ninaomba tuendelee na hiki kitu ;
“Dark websites HATARI” hufanya kazi kama Dark website salama, na hizo Dark website hatari nazo huwa zinaomba ujaze vitu kama jina, email, password ili uweze kupata unachohitaji, lakini wengi wetu hatufahamu madhara yake,
Leo nitakwambia kwa ufupi sana kuhusu wale watu Wanaoingilia account za watu wengi bila wahusika kufahamu hutumia mbinu gani,
Wao huleta kitangazo kizuri sana tena kina picha nzuri nzuri zikikwambia “download” au “open” au “get this” nawewe kweli masikini bila kujielewa unabonyeza (Unapelekwa sehemu hatari bila kufahamu), na ukiingia huko utakuta kuna sehemu zinakutaka ujisajili, na wengi wetu huwa tunajaza tu data zetu bila kuelewa tunapelekwa/zinapelekwa wapi.
Nikupe siri sasa, “Dark websites HATARI” ni website fekizinazotumiwa na wahalifu kukusanya data za watu, na mara nyingi kwa wale wanaopenda kudownload vitu wasivyovijua.
Ukiwa ndani ya Dark website hatari wala hautagundua chochote hadi uwe na software/antivirus ya kukujulisha kuwa upo hatarini, mara nyingi ukiwa humo huwa kuna mdudu anaitwa “Malware” anajidownload bila wewe kufahamu na anaingia ktk simu au Computer na anajificha.
Kazi kubwa ya huyu mdudu ni kuiba data zako muhimu na kuzituma kwa mmiliki wa hiyo Dark website Hatari, (Wataalamu wa IT wengi huwa wanaweza kuziset hizi Dark website HATARI hivyo ninaamini wananielewa vizuri)
Namna ya kuepuka;
Njia ya kwanza;
Ukiwa na simu au Computer unaweza kutumia Antivirus inayoitwa Eset Node 32 Antivirus ambayo inaprotection nyingi zikiwemo hizo za kuzuia Dark websites HATARI, kwa wenye simu mtaipata play store kwa kuandika neno “eset” na kubonyeza search/go, itatokea ya kwanza kabisa imeandikwa “Mobile Security & Antivirus” na wenye Computer mtaipata hapa ⇒  https://maxitclub.wordpress.com/antivirus-nzuri/mimi binafsi huu ni mwaka wangu wa 3 ninaitumia na nipo salama), kwa wenye Computer ninawashauri muachane na kutumia Antivirus nyingine hizo zinazowasumbua ku update kila siku.
Njia ya pili;
Epuka kupokea simu, sms na email zinazotoka sehemu zisizo julikana “Unknown sources” nafahamu wenye Smartphones mnajua hiki kitu, kuwa kuna sehemu imeandikwa “Allow installations from unknown sources”, hawa jamaa wanafahamu kila kitu na ndio maana wamekuachia jukumu ujiamulie mwenyewe.
Njia ya tatu;
Epuka kudownload au kubonyeza hovyo matangazo usiyokuwa na taarifa nayo, na mara nyingi huwa yanakuwa ni matangazo ya Ngono, Miziki, Biashara n.k, acha hiyo tabia ya kubonyeza kila uachokiona.
Hitimisho;
Hasara ya kuingia kwenye Dark Website HATARI, utakuwa unaona text au email zinaingia kila siku na nyingi huwa zinakuja na majina ya kike zikiomba ujibu na pengine mtumiane picha, au nyingine zikikudanganya kuwa kuna hela zipo sehemu hivyo basi usaidie kwa kutuma account namba yako ya benki ili zihamishiwe kwako. Walio wengi huwa wanafanya hivyo, lakini hatari yake ni kubwa, ipo siku utafanyiwa kitu kinaitwa “HACKING” kwa kiswahili ni “KUINGILIWA KWENYE ACCOUNT ZAKO BILA KUFAHAMU
Ushauri;
Kwa wafanyakazi mnaofanya kazi kwenye makampuni makubwa kama yanayojihusisha na mambo ya Fedha, Usalama, Huduma za Afya, Wahasibu Vyuoni au Mashuleni, Viongozi wakubwa na wadogo Au watoa huduma zozote za muhimu ktk jamii mnatakiwa muache kabisa tabia ya kujaza hovyo data zenu mahala msikokujua. Aidha kwa wasio wafanyakazi pia mnapaswa kuacha ili kuwa salama zaidi.

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply