Kwanza kabisa ninaomba kuanza na utagulizi kama ifuatavyo, tunapo zungumzia usafi ktk Computer tunamaanisha usafi wa aina mbili;
- Usafi wa ndani ya Mafaili na Software za Computer (Software and File checkup and maintenance)
- Usafi wa vifaa vyote vya ndani na nje ya Computer (Hardware checkup and maintenance)
Ufanyaji usafi ktk Computer yako una faida nyingi sana ikiwemo;
- Kuongeza urefu wa maisha ya Computer yako
- Kuongeza umahiri wa Computer yako ktk utendaji kazi
- Kupunguza gharama za ununuaji vifaa vilivyoharibika kwa kupuuza kufanya usafi
- Kuepusha Computer kuzimika ghafla kwa kuzidiwa na uchafu au wadudu
- Kufanya Computer iwe na spidi kama ilivyounuliwa mwanzo
Kutokufanya usafi ktk Computer yako kuna hasara zifuatazo;
- Inaweza kucrash au kufeli na kuzimika ghafla
- Spidi ndogo ktk utendaji kazi
- Kukosa umahiri ktk utendaji kazi, yaani haitakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu na itakuwa inachemka na pengine kuzimika baada ya muda mfupi
- Gharama kubwa siku ambayo Computer imeharibika sababu itakuwa imeharibu vifaa vingi
- Utakuwa umeipunguzia urefu wa maisha yake maana haitadumu hata kwa muda wa miaka miwili
Hivyo basi, usafishaji wa Computer SAHIHI, unafanywa na wanaofahamu tu yaani maexpert wa IT, na kuna mambo mengi sana yanayotakiwa kufanywa, hivyo basi kama na wewe ni miongoni mwao inabidi ufanye haraka kuwaona wataalamu.
No comments: