» » Ongeza Space Kwenye Smartphone Yako

Ninafahamu kuwa huwa unahangaika kufuta vitu lakini bado haupati space ya kutosha kuweka data zako au kuinstall applications nyingine
Yote hiyo ni kutokufahamu mambo haya ninayokwenda kuyaeleza hapa chini
Popote ulipo ninakuhakikishia utaweza kufanya hiki kitu na baada ya kukikamilisha basi utapata space ya kutosha
  1. Kamata Smartphone yako
  2. Fungua “Settings
  3. Ukiwa hapo kwenye “Settings” angalia sehemu iliyoandikwa “storage“, kama picha hii hapa chini inavyoonyesha,

  4. Max storage.pngUkiwa hapo kwenye Storage angalia kulia kwake utaona maneno kama (AppsPicturesAudiosDownloadsCached Data, na Misc au Miscellaneous Files), ninaomba nikwambie kitu, kama ulikuwa haujawahi kabisa kufika huku basi itachukua muda kidogo kucaluculate kiasi cha MB zilizopo kwenye kila neno nililolitaja, na ukiangalia vizuri kwenye picha utaona chini ya kila neno nililolijata kuna maneno yanasema “Calculating

  5. Sasa basi, ikimaliza kuCalculate itaonyesha kiasi cha MB kwa kila kimojawapo, na sisi tunaanza na “Cached Data“, unapaswa kubonyeza hilo neno “Cached data“, kisha litakuuliza kama picha hii inavyoonyesha hapa chini,

  6. Max Cached DataIkikuuliza hivyo usipate tabu, wewe bonyeza neno “OK” Kisha Subiri kwa muda wa sekunde chache hadi hilo neno “Cached data” lipotee

  7. Pia ninaomba nikwambie kuwa, kama, baada yakucaluculate kiasi cha MB ulikuta, kwa mfano hapo kwenyeCached data yangu ni MB 42.11, sasa tuchukulie kwako ulikuta MB 600, basi ujue hizo MB 600 zilikuwepo ila haukuwa na uwezo wa kuzitumia (kwa lugha nyepesi zaidi)

  8. Sasa tuendelee
  9. Baada ya lile neno “Cached data” kupotea,
  10. Angalia hapo hapo kwa juu kuna sehemu imeandikwa “Available” au kwa wengine mtakuta “Available space” utaona space iliyowazi imeongezeka, sijamaliza bado

  11. Baada ya Kumaliza hiyo, sasa rudi kwenye settings halafu tafuta sehemu imeandikwa Apps au Applications, ukiipata ibonyeze na utaona zimefunguka pembeni,
  12. Baada ya Hapo, bonyeza Application moja baada ya Nyingine, na kila baada ya kufungua App moja utakuwa unakuta neno “Clear Data” basi uwe unabonyeza hilo neno “Clear Data
  13. Fanya hivyo kwa kila App unayoiona hapo, na hakikisha kila baada ya kuclear data inabaki na MB sifuri
  14. Na mwisho kabisa Angalia tena hiyo sehemu iliyoandikwa “Available au Available space” utaona ongezeko la MB
Ninaomba nikupe ushauri juu ya hili zoezi,
Unapaswa kulifanya mara kwa mara kwa sababu, unapofungua mitandao ya kijamii kama, Facebook, InstagramTwitter, na kadhalika, au unapokuwa unatumia browsers kama Mozilla,OperaUc, na kadhalika, huwa vinatunza kitu kinaitwa history, yaani mambo uliyoyafanya huko nyuma, na kwa kiasi kikubwa sana vitu hivi huficha MB nyingi sana bila sisi wenyewe kufahamu, na ndio maana huwa tunahangaika kufuta vitu lakini bado hatupati MB za kutosha.

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply