» » WhatsApp ktk Computer

WhatsApp isiyosumbua na bora kutumia katika computer yako.

Wengi wetu tumezoea kutumia Whatsapp kwenye Computer ambayo imo ndani ya Software iitwayo BlueStacks, kwa namna moja au nyingine huwa unajionea tabu na usumbufu unaoupata wakati wa kuingia ktk Whatsapp yako.
Sio hivyo tu, hata wakati unatumia hiyo whatsapp iliyo ndani ya Bluestacks unaona kama Computer inafanya kazi taratibu sana, hilo ni moja ya tatizo lisababishwalo na Bluestacks (Computer kuwa slow).
Sasa leo hapa nakuletea mzigo mdogo tu, yaani whatsapp iliyo single kutumika ktk Computer kama namna unavyotumia program zingine.
Whatsapp hii ina ukubwa wa MB 57 tu, na inakuwa installed kama kawaida, yaani kama unavyoinstall software zingine.

Sasa basi tuelewane ktk hili kidogo;

  1. Kwa wale wenye windows 8 hadi 10, hakuna tabu mtainstall bila kudownload kitu kinaitwa NetFramework 4.
  2. Kwa akina sisi ambao tuna windows 7 wakati tunaanza kuinstall whatsapp yetu itatuomba kwanza ifanye installation ya NetFramework 4.5, hivyo basi unachotakiwa kufanya unga Computer ktk mtandao halafu install whatsapp, ikikuuliza kama unairuhusu idownload netframework 4.5 ikubalie kisha kuwa mpole tu itamaliza baada ya muda mfupi kisha itakuomba irestart Computer we ikubalie tu halafu fuata hatua zifuatazo;

Hatua za kuinstall

Hii ni kwa wote sasa, wenye windows 8, 8.1, 10 na sisi wenye 7 tuliomaliza kuinstall netframework 4.5
  1. Download software kupitia link ninayokupa hapa chini
  2. Ukishadownload, fungua hilo folder na ndani yake utakuta setup ya Whatsapp
  3. Doubleclick hiyo setup tayari kwa kuinstall, itakuomba password
  4. Jaza “maxitclub” bila alama za fungua na funga semi kisha bonyeza ok na endelea na installation
  5. Kama nilivyoeleza awali, wale wa windows 8, 8.1 na 10 mtaendelea na installation ila wale wa windows 7 mtaombwa kuinstall netframework 4.5 hivyo mfuate maelezo niliyotoa hapo juu
  6. Baada ya kuinstall itaweka kijishortcut chake cha whatsapp ktk desktop na itafungua menu ya awali ya whatsapp
  7. Kwenye menu ya awali utaona kitu kama kina draft ya rangi nyeusi na nyeupe yenye alama ya whatsapp katikati, angalia kwa makini sana.
  8. Sasa zoezi hili la mwisho ni kuactivate whatsapp yako ktk Computer
  9. Kamata simu yako yenye whatsapp
  10. Kisha fungua whatsapp na angalia juu kulia utaona vijibutton vitatu yaani vile vya option (kule huwa ukitaka kubadili status unabofya) basi vibonyeze hivyo vibutton vitatu
  11. Kisha vitatokea vijioption vingi vingi
  12. Bonyeza sehemu imeandikwa web au whatsapp web
  13. Baada ya kubonyeza hapo utaona kitu kama camera kimewaka kwenye screen na kina mstari unaopanda na kushuka
  14. Sasa basi elekeza hiyo Camera kama unataka kupiga picha pale kwenye computer kwenye lile dude lenye draft nyeusi na nyeupe lenye alama ya whatsapp katikati
  15. Hakikisha umeelekeza kamera vizuri ili uweze kuscan na kuactivate whatsapp yako
  16. Kama umeweka inavyotakiwa basi hata sekunde 10 haziishi utakuwa umeactivate whatsapp yako na kuanzia hapo unaweza kuanza kutumia single app yako ya whatsapp ambayo ni nyepesi kuliko kufungua hata Microsoft word
  17. Ukizima computer na baadae ukiwasha basi whatsapp yako utaikuta vile vile kama mwanzo na icon yake itakuwepo ktk desktop na kwa kawaida tu ni kwamba pindi uwashapo data kwenye simu yako basi na whatsapp kwenye computer itakuwa active
  18. Ukiweza kuinstall kama nilivyokuelekeza basi utafurahi mwenyewe maana ni zaidi ya haraka
Kama kawaida nakupa mzigo kamili kupitia link hii hapa chini;
Bofya hapa kudownload whatsapp yako;
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD SOFTWARE HII

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply