» » Maswali ya Kujiuliza Unapotaka Kununua Simu



Iwe unataka kununua simu mpya au iliyotumika ni muhimu kujipanga kwani mara nyingi ukishanunua ndiyo umenunua kunakuwa hakuna kubadili uamuzi tena. Na tukubaliane wote ni mara chache sana mtu unanunua simu ili ubadilishe baada ya wiki mbili tatu, tunanunua simu ilituzitumie muda mrefu kidogo.
1. Je nataka simu ya kawaida au nataka smartphone?
Kama unaitaji kununua simu kwa ajili ya kupiga na kupokea simu tuu, pamoja na kutuma meseji kwa mfumo wa kawaida wa SMS basi huna sababu ya kupoteza pesa nyingi kwa ajili ya kununua smartphone.
Ni rahisi sana kufanya chaguzi pale unapotaka kununua simu ya kawaida. Ugumu ni pale unapotaka smartphone. 
Kwenye smartphone inabidi ujiulize ni kiwango gani cha ubora wa kamera, RAM, Diski uhifadhi (memori) n.k, pia ubora huo ulinganishe na bei. Kwenye kununua smartphone mara nyingi suala litakuja kwenye bei na aina ya sifa ya simu unayotafuta. Pia kumbuka kuwa ili kufaidi smartphone basi lazima uwe tayari kuingia gharama za data za intaneti kila mara.
2. Je ukubwa/umbo lake ni zuri kwangu?
Ndiyo… ili ni swali muhimu kujiuliza. Hapa angalia ata jinsi gani simu hiyo inakaa kwenye kiganja chako. Wengine wanaviganja vidogo na uhakika msimu mnene na mpana utakusumbua pale unapopiga au kupokea simu. Ila pia kama nguo zako ni za ‘kimodel’ inamaanisha ukitaka simu kubwa basi pia itabidi uwe na kabegi au pochi ya kuibebea hiyo simu.
3. Ubora wake na aina ya kazi au mazingira unayoishi
Ni sehemu muhimu kuangalia. Hapa namaanisha unafanya kazi ya aina gani? unaishi mazingira ya aina gani? Hii ni muhimu kwani kama mazingira ya kazi unapoishi kunaweza kuwa ni eneo la kitu kuweza anguka mara kwa mara basi hakikisha unanunua simu ambayo ata ikianguka mara 5-10 kioo chake bado kinakuwa imara. Pia kama eneo la kazi ni rahisi wewe kulowa lowa mara kwa mara basi unaponunua simu ata kama ni smartphone chagua zile zenye uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani kwa uraisi – yaani ‘water-resistant’

4. Intaneti gani inatumia?

Hapa kama huna shida ya intaneti sana na utumiaji wako ni mdogo basi utaweza kununua simu zenye 2G ila siku hizi zipo chache sana. Simu nyingi hasa smartphone zinakuja na teknolojia ya 3G, hii ndiyo ni kasi zaidi ya 2G. Ila pia kuna simu nyingi kutoka nje zilizotumika huwa zinauzwa nchini na baadhi ya simu hizo zinakuwa zimetengenezwa kwenye mfumo wa teknolojia ya 4G ambayo ni ya kisasa zaidi, fahamu mapema kwa sababu mitandao yetu mingi bado hawatumii teknolojia hii. Zipo zenye teknolojia zote mbili ila pia zipo zenye 4G pekee, hivyo chunguza vizuri.
5. Je kioo chake kinanitosha?
Ukubwa wa kilo, yaani ‘display’, huu upimwa katika inchi. Basi angalia na uridhike nao, pia omba simu hiyo iwashwe na uangalia kiwango cha ubora wa kioo icho simu ikiwa imewaka. Je vitu vinaonekana vizuri? Pia kama ni simu ya kuandika kwa mguso (touchscreen), je inagusika vizuri? Kwani kuna vioo vingine vinakuwa ni vya ubora mdogo na vitakusumbua katika kuandika.
Pia fuatilia je kioo kinaonesha vitu vizuri ata pale kinapopigwa mwanga wa jua, kwani simu zingine hazisomeki kabisa kwenye mwanga wa jua.
6. Je ni Programu Endeshaji (OS) gani inanifaa?
Siku hizi kazi ni kwako, kuna Android, iOS – Apple, Windows, BlackBerry OS, Firefox OS, na zile za kichina. Fahamu ni ipi unaipendelea zaidi na ipi inaweza kukupa apps unazotaka. Kwa sasa Android na iOS ndio zenye apps nyingi zaidi.
7. Je ni rahisi kuitumia?
Ndiyo, kuna simu ambazo mtu hauitaji miezi kujifunza kutumia na kuna zile ambazo kama sio mtundu sana basi utahangaika nazi sana. Hii inaweza ikawa kwenye mfumo wa kibodi zake au muonekano wake tuu na jinsi walivyoweka mambo ndani yake. Ili ni swali muhimu vinginevyo utajikuta unaomba watoto wadogo wakusaidie kuandika meseji kila siku 🙂
8. Je inatengenezeka? Huduma kwa wateja!
Kuna makampuni mengine ya simu huwa yanamaofisi na utaweza kupata matengenezo pale simu yako ikiwa na tatizo au ikashindwa kufanya kazi ghafla ndani ya muda mfupi. Pia kuna simu ambazo ata ikiharibika kioo ni raisi wewe kwenda kwa fundi na kuweza kukibadilisha ila pia zipo simu ambazo hazina spea, yaani ata betri yake ikiharibika kupata jingine ni vigumu. Ulihangalie ili pia pale unaponunua simu mpya.
9. Je ina kamera nzuri? Je kuna apps nyingi?
Haya maswali nimeyaweka pamoja kwani yote yanaingiliana kidogo, yote utakutana nayo kama utataka kununua smartphone. Tuanze na kamera, kipimo cha ubora wa kamera ni ‘pixels’, kama unapenda kupiga picha sana basi ujue kiwango unachoitaji cha MegaPixels kisipungue 10, ila pia hili litaendana na kiwango cha pesa ulichonacho. Pia siku hizi ata simu za kawaida ambazo zinakuwa na kamera, unaweza pata simu za bei rahisi zikiwa na kamera ya kiwango cha MegaPixel 3 na ata zaidi.
Apps? Suala la apps kama unanunua simu inayoangukia kwenye Android, Windows, iOS na ata OS zingine si suala kubwa sana. Ila Android na iOS ndizo zinazoongoza zaidi kwa apps.
10. Je betri yake inadumu muda gani?
Kama maisha yako ya kila siku unaweza kuchaji simu mara 2-3 kwa siku bila kulalamika au wewe unaitaji simu inayoweza kudumu na chaji siku 2-3 ili ni muhimu kujiuliza. Pia unavyojaza apps nyingi zaidi kwenye simu bila ya msingi na kuzitumia ndivyo ulaji wa chaji unaongezeka zaidi.
11. Je mfukoni una’Sh ngani?
Hahahahahha… ndiyo ili nalo muhimu! Kumbuka kama una bajeti kubwa basi unaweza kununua simu ya kiwango cha juu zaidi lakini ili pia linategemea maamuzi yako kutokana na maswali yaliyotangulia.

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

1 comments:

  1. Harrah's Philadelphia Casino and Racetrack - JT Hub
    Harrah's Philadelphia 상주 출장안마 Casino and Racetrack is located in Chester, PA at 777 구미 출장안마 Harrah's Blvd. 광명 출장마사지 Save big 하남 출장마사지 with JT Hub. 세종특별자치 출장마사지

    ReplyDelete