» » Jinsi ya kuweza Ku unlock moderm yako na kuanza kutumia laini zote (universal)

Habari gani mpendwa karibu tena katika jukwaa letu ili uwEze kupata hiki Na kile juu ya teknolojia Kwa lugha ya kiswahili....  karbu uendelee Na maada yetu ya Leo ambayo itakupa mwanga Wa Jinsi gani utaweza Kufungua moderm yako kutoka kutumia laini moja hadi kuwa universal Twende pamoja SASA...



Kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya intaneti kumepelekea makapuni ya simu za mikononi kubuni matumizi ya modem kwa ajili ya kuweza kupata huduma ya intaneti.


Ingawa kuna makampuni mengi ya simu na kila kampuni ina modems zake na ushindani pia kuchukua nafasi yake kwa kila kampuni kuwa na huduma ya vifurushi vitakavyowavutia wateja. Suala la kujiuliza ni je, utakuwa na modem kutoka kila kampuni kwa sababu huduma zao zimekuvutia? Hapana, jambo la kuzingatia ni kuwa na modem moja ambayo itakuwezesha kutumia line yoyote.


Hapa nitakuelekeza kwa kutumia Huawei E173, fuata maelekezo kulingana na aina ya modem yako.

moderm ya Huawei

Jinsi ya ku-unlock Huawei E173 modem

Pakua programu wezeshaji iitwayo  Huawei ‘Mobile Partner‘ kwa ajili ya Windows OS kama unatumia Windows kwenye kompyuta yako. Baada ya kupakua ‘right click’ kisha bofya ‘Run as administrator‘. Kisha fuata maelekezo mpaka mwisho na kuistall.
  1. Weka sim card kwenye modem ambayo ni tofauti na kampuni ya simu; kama ni modem ya Airtel weka sim card ya Tigo, Voda, n.k ila sio line ambayo ni kutoka kampuni hiyohiyo inazotoa modem unayotumia kisha subiri mpaka iwe detected. Usiinstall programu (mobile partner) iliyokuja na modem.
  2. Pakua na kuinstall DC Unlocker ya hivi karibuni. Kisha ifungue na kuchagua ‘Huawei‘ pia, chagua ‘Auto detect(recomended)‘ kisha bofya kitufe cha kutafuta(search).
  3.  Funga mobile partner pamoja na DC Unlocker kisha download Firmware toleo la hivi karibuni. Ondoa mafaili hayo katika mkusanyiko wa pamoja(zip) kisha right click kwenye setup na ifungue kama administrator. Install mpaka mwisho wa mchakato mzima wa installation..
  4. Restart DC Unlocker. Kisha ifungue na kuchagua ‘Huawei‘ pia, chagua ‘Auto detect(recomended)‘ kisha bofya kitufe cha kutafuta(search). 
  5. Ili kuweza kufungua modem yako inabidi ulipie pesa kidogo kama Tsh 9,000 kwa kutumia Paypal kisha bonyeza severs kuweza kuweka username na password ambayo utatumiwa kwenye email address yako.
  6. Bonyeza ‘Unlock‘ kisha chagua ‘Read Unlock Code and auto enter to modem‘ halafu bonyeza ‘Do job‘.
  7.  Bonyeza sehemu ya kutafuta(search) kuhakiki kama modem yako imefunguka na utaona sehemu ya ‘Sim lock status‘ imeandikwa imefunguliwa (unlocked).
Kwa kufuata hatua hizo utakuwa umeweza kufungua modem yako na kuweza kutumia sim-card yoyote kwenye modem yako? Je, umefanikiwa ku-unlock? niambie katika comment.
☆☆Ahsante Na karibu tena upate mwanga kuhusu technology☆☆☆

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

2 comments: