» » Ongeza Spidi ktk Smartphone/Tablet Yako

Je unapenda Smartphone au Tablet yako ifanye kazi kwa spidi kama ya Usain Bolt? Je unajua nini cha kufanya? na je unajua kama wewe mwenyewe unaweza kuiongezea spidi Smartphone/Tablet yako? Hebu soma kwa makini kisha fuata maelekezo yote niliyotoa hapa.
Kama simu/tablet yako inatumia Android basi tuendelee, na kama ni wale wa Windows phone na Iphone basi msome kwa faida yenu tu.
Ok, tutaenda moja kwa moja,
Kama Simu/Tablet yako huwa inakusumbua sana kwa mambo yafuatayo;
  1. Ukifungua Program zako inachelewa sana
  2. Ukifungua hata Contacts zako inachelewa sana
  3. Ukifungua sms umtumie mtu inachelewa
  4. Ukiiwasha inachelewa
  5. Yani kwa kifupi ishakuchosha maana hata ukipunguza vitu mwendo ni uleule kama trekta
Basi usijali, leo umekutana na daktari, ninakupa maujuzi na unaishughulikia hapo hapo ulipo;
Sasa basi, ili uweze kugundua hivi vitu lazima uwe na utaalamu kidogo juu ya haya mambo, ninaamini kwetu waTanzania Tulio wengi ni vigumu sana kusoma hivi vitu kwa faida zetu binafsi, na ukizingatia vinakuwa katika lugha ya kigeni, lakini ukiwa unanifuatilia vizuri basi tutaenda na lugha yetu hii hii ya Kiswanglish.
Maana ya kusema hivyo ni Kwamba;
  1. Lazima ujifanye kama nawewe ni mtaalamu wa haya mambo ili kutatua tatizo la simu/tablet kufanya kazi kwa spidi ndogo
  2. Halafu uwe mjanjamjanja kuzitumia hizo njia za kuifanya simu/tablet yako iwe na spidi ya kushangaza
  3. Hizi option za kufanya yote hayo, huwa zimo kwenye simu/tablet zetu lakini zimefichwa na hazionekani na kama hukuelekezwa vizuri hautaweza kuzitumia
  4. Sasa ili kuzifanya hizo option za kitaalamu zionekane na ili tuweze kuzitumia, inabidi tuzifichue kwanza
  5. Sasa kamata simu yako twende pamoja
Hatua ya kwanza ni Kufichua Option za kitaalamu (Developer Options)
Hapa ninafahamu wapo wanaoelewa kwa haraka na wapo wanaoelewa kiasi na pia wapo ambao masikini hawaelewi kabisa, kwa hiyo mie nitachukulia kama ninaelekeza wale ambao hawaelewi kabisa ili nisimuache mtu.
  1. Ninaamini umekamata Smartphone/tablet yako
  2. Kwanza kabisa kama umesha enable hiyo option ya kitaalamu (Developer option) basi utulie kwanza, na kama haujui kitu basi twende pamoja 
  3. Baada ya kukamata smartphone/tablet yako, ingia kwenye “Settings
  4. Halafu shusha/Scroll hadi chini kabisa kule kwenye “about phone” au “about tablet

    Max android-about-phone
  5. Usibonyeze kitu, maana wengine wanaharaka kama nini,
  6. Hebu angalia hapo kwa kutokea chini kwenye hiyo “about phone” kupanda juu utaona kuna option nyingine juu ya hiyo “about phone
  7. Sasa nisikilize vizuri
  8. Kama unaona ipo option imeandikwa “Developer Options” basi tulia kwanza usubiri wenzako
  9. Kama haujaiona, kama hiyo picha inavyoonyesha hapo maana yake bado hiyo option ya “Developer Options” imefichwa na hauwezi kuiona hadi tuifichue kwanza
  10. Kwa wewe ambae hiyo option haipo lazima kwanza utakuwa ulishakumbwa na matatizo kama (simu kugoma kusoma USB Cable), (Simu kuwa na Spidi ndogo), (Simu kuchagua chagua chaji) na mengine mengi tu, sababu haukuwa unafahamu
  11. Sasa basi twende tukaifichue hiyo option,
  12. Ukiwa hapo hapo kwenye “about phone
  13. Bonyeza hilo neno “about phone
  14. Utaingia sehemu kama hii hapa kwenye picha,

    max android-tap-build-number
  15. Na hapa nataka utafute kitu kimeandikwa “Build number
  16. Kama umekiona ninashukuru sana
  17. Sasa tutafanya kamchezo kamoja hapa, andaa kidole chako chenye spidi
  18. Eti wengine wameandaa dole gumba, tumia kidole kingine wewe
  19. Haya sasa fanya hivi, bonyeza hapo kwenye neno “Build number” mara nyingi nyingi halafu haraka haraka sana hadi uone simu imekwambia “You are now a developer!
  20. Ukiweza tu, kwanza relax, halafu jiulize hivi kwanini wazungu wanatutesa hivi
  21. Haya sasa tuendelee baada ya kurelax
  22. Baada ya kuambiwa “You are now a developer!” yaani maana yake ni “sasa umekuwa mtaalamu kuifanya simu yako unavyotaka”, naomba sasa turudi pale kwenye settings kisha tushuke chini kule kwenye “about phone” au “about tablet” tutaikuta option yetu imeongezeka inaitwa “Developer options” kama picha yetu inavyoonyesha hapa chini,

    Max android-open-developer-options
  23. Sasa basi, hapa wote tupo pamoja, yaani wale tuliokuwa tunayo, ambao hatukuwa nayo, tunaoelewa sana, tunaoelewa kiasi, na tusiojua kabisa
  24. Twende pamoja sasa, hebu bonyeza hiyo “Developer options
  25. Itakupeleka kwenye vitu vingi sana mpaka unaweza kuhisi kuchanganyikiwa
  26. Unachotakiwa kufanya ni kufuata kile ninachokuelekeza
  27. Ninaomba ukiwa hapo shuka chini/scroll hadi upate maneno uzipate sentensi tatu zilizoandikwa hivi (Window animation scale, Transition animation scale, na Animator duration scale) kama picha hii hapa chini inavyoonyesha,

    Max android-developer-options-animations
  28. Kama huwa unakula mchicha basi macho yako yatakuwa mazuri kutazama hiyo picha na kugundua kwa kila neno moja kwa yale niliyoyataja hapo namba 27 (Window animation scale, Transition animation scale, na Animator duration scale) , chini yake kuna maneno haya (Animation scale 1×)
  29. Kama umeyaona basi vizuri, sasa ninaomba nichukue nafasi hii kukueleza kuwa hivyo vitu vitatu hapo kuwekwa kwenye scale kubwa kama hiyo ya saizi ya moja (1) ndivyo vinafanya simu au tablet zetu kufanya kazi kwa spidi ndogo
  30. Sasa basi tunachotakiwa kufanya hapa ni hiki,
  31. Anza kwanza kubonyeza hiyo “Window animation scale”kisha itafunguka kama picha hii hapa chini inavyoonyesha

    Max turn-off-android-animations
  32. Ikifunguka hivi tu basi hapo kwenye hiyo option unatakiwa uchague “Animation off” na sio kuchagua (Animation scale 1×)
  33. Basi kwa option zote tatu chagua Animation off na hakikisha zote zinasoma hivyo
  34. Baada ya hapo, rudi kule kwenye “settings
  35. Sasa tunakamilisha zoezi letu kwa kufanya kitu hiki
  36. Ukiwa hapo kwenye “settings” tafuta sehemu iliyoandikwa “Apps” au “Applications” na baada ya kuiona basi ibonyeze,
  37. Ukiibonyeza itakupekeleka sehemu ya applications zako zilizo kwenye simu au tablet yako
  38. Ninaomba unisikilize kwa makini sana
  39. Ukiwa hapo kwenye Hizo applications angalia juu kabisa utaona neno “Downloaded
  40. Maana yake upo upande wa applications ulizozidownload mwenyewe, kitu ambacho hatukihitaji sisi kwa sasa, kwa hiyo unatakiwa uzisukume hizo applications kuelekea kushoto kama unazislide vile, na ukizisukuma kwa mara ya kwanza utaona kule juu kabisa kulikoandikwa “Downloaded” kunabadilika na kuwa “Running“, kwa mara nyingine tena zisukume kuelekea kushoto, kutabadilika na kuandikwa “All
  41. Na hapo ulipofika ndipo tunaenda kumalizia kazi yetu
  42. Ukiwa hapo shuka shukashuka chini huku unatafutaApplication iliyoandikwa “Launcher” kama picha hii inavyoonyesha hapa chini,

    Max android-manage-launcher-app
  43. Endapo utaikosa “Launcher” basi badala yake unaweza kurestart simu yako (yaani mbadala wa kutumia Launcher ni kurestart simu au tablet yako0)
  44. Ila kama utaipata “Launcher basi ibonyeze na ukiibonyeza tu itakufungulia sehemu nyingine kama picha hii hapa chini inavyoonyesha,

    Max restart-android-launcher
  45. Ikikupeleka hapo, basi bonyeza neno “Force stop”
  46. Itakuuliza “If you stop an application, it may misbehave” unachotakiwa kufanya ni kubonyeza “ok”
Baada ya hapo sasa rudi na tumia simu yako, jaribu kufungua vitu vyako kisha pima spidi yake, utaona ni zaidi ya magari ya mwendo kasi.
Mjulishe mwenzako kuwa hapa kila siku kuna mambo mapya hivyo asikose kutembelea site yetu, kuhusu Comments ninaomba ukoment kupitia facebook, na kwa wale mlio mikoani pitia kila kitu kwenye site hii kisha njoo inbox tuyajenge, ninafundisha tuition za Computer kwa faida binafsi kwa bei poa tu kupitia WhatsApp inbox.
Karibuni

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply