Mara nyingi ubovu wa hizi power supply hutokana na mambo yafuatayo;
- Kufungua Desktop Computer kusafisha na kukosea kuunganisha nyaya zake
- Computer kuzimika ghafla kutokana na joto kuzidi ndani ya system unit
- Umeme kukatika na kurudi kwa kasi
- Shoti ya umeme kupiga kwenye Computer
- Kufa kwa feni ya ndani ya power supply na kusababisha kupanda kwa joto ndani yake
- Kuchezea swichi nyekundu ya power supply iliyopo nyuma yake
Masomo Haya Hufundishwa vyuoni tu, tena sio vyuo vyote, hivyo basi tutaanza kama ifyatavyo;
Tunapozungumzia Power supply tunamaanisha kitu hiki hapa chini kwenye picha;
Hizo ndio power supply tunazo zungumzia, sasa basi hapa inabidi kufahamu kwa kina maana, aina ya hizi power supply pamoja na kazi zake
Tukianza na maana;
Hiki ni chombo/kifaa kinachofua na kubadilisha umeme kutoka kwenye Ampia (hasa ule wa kwenye soketi za umeme za ukutani) kwenda kwenye volteji (umeme uliobadilishwa/kupunguzwa hadi kufikia kiwango kidogo kinachoweza kugawanywa kwenye vifaa vya ndani vya Computer kama RAM, PROCESSOR, FENI, MOTHERBOARDnakadhalika
Sasa tunaingia kwenye aina;
Ili kutambua aina ya hizi power supply huwa tunaangalia idadi ya matundu kwenye nyaya zake kubwa zinano ingiza volteji (Volts) kwenye Computer
Hapa nitaelezea kwa kina kidogo, Hebu angalia picha hii hapa chini;
Kwa umakini wa hali ya juu sana ukiangalia hizo nyaya utaona kuna hiyo nyeupe kubwa kuliko zote, sasa basi hiyo kubwa au ndefu kuliko zote ndio huwa tunatumia kutofautisha aina za hizi power supply
Yaani ukishika hizo nyaya zenye hiyo connector kubwa/ndefu nyeupe utaona matundu yenye vipini vidogovidogo vya chuma, ukihesabu hayo matundu utakuta idadi yake ni 20 au 24
Kwa hivyo basi, kama hiyo connector kubwa/ndefu nyeupe ina matundu 20 basi aina ya hiyo power supply kwa kingereza itaitwa “ATX 20 pin Power Supply” na kama hiyo connector kubwa/ndefu nyeupe ina matundu 24 basi aina hiyo ya power supply kwa kingereza itaitwa “ATZ 24 pin Power Supply”
Kwa hiyo kwa ufupi tuna aina kuu mbili za power supply, nazo ni;
- ATX 20 pin Power Supply
- ATZ 24 pin Power Supply
Sasa basi baada ya kufahamu namna ya kutazama na kuweza kutambua aina ya hizi power supply sasa tuangalie kwa kina kazi zake;
Kama inavyofahamika kuwa nadani ya Computer/system unit kuna vifaa kama, Feni ya kupoza Procssor, Feni ya kusawazisha kiasi cha joto cha ndani ya Computer, RAM, CPU, Midomo ya kusomea cd/dvd, kuna kadi za magemu, kadi za sauti, kuna hard disk, kuna taa zinazoonyesha kama Computer imewaka na vingine vingi tu, sasa basi vifaa vyote hivi vinategemea umeme kutoka kwenye Power supply, kwa hivyo basi, kumbe Power supply inakazi kubwa ya kupokea umeme kutoka kwenye soketi za ukutani au kwenye extension na kuubadilisha ili ukatumike kwenye vifaa vya ndani vya Computer
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, kumbe power supply ikifa tu/ikishindwa kufanya kazi basi na Computer yako haitaweza kufanya kazi
Endapo utakumbwa na tatizo la Desktop Computer yako kugoma kuwaka, ikiwemo kugoma hata kuonyesha indiketa zake kama inawaka basi unatakiwa upime Power supply ya Computer yako kama nzima
Tunapima vipi Power supply za Computer zetu kama ni nzima au mbovu?
Kama uliangalia aina ya power supply ya Computer yako ukagundua kuwa ni aina ya zile zenye matundu 24 kenye connector kubwa/ndefu nyeupe (yaani ATX 24 pin Power Supply) basi ili kuipima kama ni nzima au mbovu fuata hatua zifuatazo;
- Chukua kipande cha waya na ukikunje kama herufi “U”
- Kisha kichomeke hapo kwenye connector kubwa/ndefu nyeupe kwa juu ili kiunganishe waya wa KIJANI na MWEUSI, angalia picha hapa chini;
- Kisha baada tu ya kumaliza kufanya hivyo basi chomeka ule waya unaotoka kwenye soketi ya ukutani na uingize kwenye power supply kama kawaida, tazama picha hii hapa chini;
- Baada ya kuchomeka huo waya sasa basi angalia kama feni ya ndani ya hiyo power supply inazunguka
- Kama feni hiyo inazunguka basi hiyo power supply ni nzima (Computer itakuwa na tatizo tofauti na Power supply)
- Kama feni hiyo haizunguki basi hiyo power supply ni mbovu na unatakiwa ubadilishe
Kama uliangalia aina ya power supply ya Computer yako ukagundua kuwa ni aina ya zile zenye matundu 20 kenye connector kubwa/ndefu nyeupe (yaani ATX 20 pin Power Supply) basi ili kuipima kama ni nzima au mbovu, fuata hatua zifuatazo;
- Andaa nyaya mbili zilizokunjwa kwa herufi “U”
- Kisha zidumbukize kwenye matundu yenye nyaya za rangi zifuatazo
- Nyaya moja ya mkunjo wa “U” iunganishe nyaya ya KIJANI na NYEUSI kama mwanzo na hapohapo nyaya nyingine iunganishe nyaya ya PAPO(PUPLE) na NJANO
- Tazama picha hii kuelewa vizuri;
- Baada ya kuchomeka hizo nyaya sasa basi angalia kama feni ya ndani ya hiyo power supply inazunguka
- Kama feni hiyo inazunguka basi hiyo power supply ni nzima (Computer itakuwa na tatizo tofauti na Power supply)
- Kama feni hiyo haizunguki basi hiyo power supply ni mbovu na unatakiwa ubadilishe
Ninaomba kumalizia kwa kusema kuwa huu ukurasa ni kwa ajili ya pracical za Kina sana hivyo kama wewe ni Mpenzi wa IT iliyokwenda deep basi ninakukaribisha
No comments: