Ni kwa mara nyingine katika page nyingine;
Karibu sana mpendwa mpenda kufahamu mengi kuhusu ukuaji wa teknolojia, hivyo basi bila kupoteza sekunde ninaomba nianze kwa angalizo;
Muundo wa Software hii ni mmoja na ni uleule yaani inayotumika kwenye simu na inayotumika kwenye Computer hazina tofauti, hivyo basi baada ya maelezo juu ya namna ya kuinstall na namna ya kuongeza chaneli, chini/mwisho wa page nitaweka link mbili, moja kwa ajili ya kudownload software kwa watakao tumia simu na ya pili ni kwa ajili ya kudownload software hii kwa watakao tumia Computer.
Jambo kubwa hapa ni kuelewa utaratibu mzima, kuanzia kuinstall, kuongeza chaneli hadi kuangalia hizo chanel ulizoongeza na baada ya kuelewa hayo basi unaweza kuwa mtaalamu zaidi na pengine ukaja kutufunza yaliyo mapya;
- Hatua utakazotumia kuinstall kwenye Computer ni sawa na atakaeinstall kwenye simu
- Hatua za kutafuta chaneli ni zilezile (kwenye simu na Computer zote ni sawa) lakini inahitaji umakini wa hali ya juu sana, nitakuonyesha hatua hizi kwa picha
- Sasa basi utadownload hiyo software kwa kubonyeza link nitakazotoa hapo chini (Ya Computer ina saizi ya MB 84 na ile ya simu ina saizi ya MB 34)
- Kisha utafanya Installation, anaetumia simu atainstall kama kawaida na anaetumia Computer atainstall kama kawaida
- Baada ya kufanya Installation kwa ukamilifu Utaona shortcut imekuja kwa Jina la “Kodi” (jina la hii software), basi fungua hiyo software/Kodi kwa kudoubleclick hapo kwenye shortcut yake ktk desktop (kwa wenye Computer) au bonyeza icon ya Kodi ktk screen ya simu yako (kwa wenye simu)
- Baada ya kufungua itakuja na muonekano ufuatao, katika picha namba Moja,
- Sasa tunaanza hatua za kuingiza chaneli zetu, na hapa nitatolea mfano chaneli mbili tatu hivi ili nieleweke vizuri.
- Kutoka picha namba moja hapo juu unatakiwa ubonyeze neno Videos, na kitatokea kitu kama hiki hapa chini kwenye picha namba mbili,
- Kutoka kwenye picha namba mbili hapo juu, baada ya kitu hicho kutokea unatakiwa kubonyeza “OK” ili kuendelea, naamini hiyo “OK” inaonekana vizuri sana, na ukiibonyeza tu hiyo “OK”, basi kitatokea kitu kama hiki hapa chini ktk picha namba tatu,
- Ukiangalia vizuri picha namba tatu, utaona kuna sehemu imeandikwa “Video add-ons”
- Basi unatakiwa ubonyeze hapo ili kuingia ktk uchaguzi wa chaneli mbalimbali, na ukibonyeza hapo, basi kitatokea kitu kama hiki hapa chini kwenye picha namba nne,
- Kutoka picha namba nne unatakiwa kubonyeza hilo neno “Get more…“, na ukibonyeza tu utaona kinatokea kitu kingine kama hiki hapa chini kwenye picha namba 5,
- Kutoka picha namba 5 utajionea chaneli nyingi sana zimeorodheshwa hapo, sasa mie nimeamua nitolee mfano namna ya kuiongeza na kuiangalia chaneli ya ALJAZEERA.
- Kwa hiyo utachagua chaneli unayoitaka kwa mfano mimi nimechagua hiyo ALJAZEERA na nikaibonyeza,na baada tu ya kuibonyeza kikatokea kitu kama hiki hapa chini kwenye picha namba sita,
- Kikitokea kitu kama hicho hapo kwenye picha namba 6 kitakuomba ufanye installation ya hiyo chaneli uliyochagua, kwa hiyo utabonyeza neno “Install“
- Na hapo itadownlod hiyo add on ya chaneli uliyochagua kwa muda wa kama sekunde 10 kisha itakuletea screen kama hii hapa chini kwenye picha namba saba,
- Ukichungulia vizuri Utaona neno “Enabled” kulia mwa nenoALJAZEERA, maana yake hapo umeshadownload hiyo add on ya chaneli uliyochagua na imesaviwa tayari.
- Sasa basi kama unahitaji kuiangalia itakulazimu uibonyeze hapo kwenye jina lake, kwa mfano mimi nitabonyeza nenoALJAZEERA, na baada ya kubonyeza tu italeta kitu kingine kama hiki hapa chini kwenye picha hii namba nane,
- Kama una macho mazuri utakuwa umeona neno “Open“hapo kwenye rangi ya blue, nadhani ndipo unapotakiwa kupabonyeza, na ukipabonyeza tu kitatokea kitu kama hiki hapa chini ktk picha namba tisa,
- Sasa basi kutoka picha namba 9 hapo juu utaona neno “Watch live” na ukipabonyeza hapo tu, basi utaenda moja kwa moja ktk chaneli yako, kwa mfano mimi nitaenda moja kwa moja ktk chaneli ya ALJAZEERA na kuanza kuangalia live kama picha namba 10 inavyoonyesha hapa chini,
- Sasa basi kabla sijatoa link za kudownload hizi software naomba nikueleze jambo moja, ukitaka kuongeza chaneli nyingine basi utafuata hatua hizo hizo kama nilivyoiongeza ALJAZEERA, ninamaana kuwa utatakiwa kurudi mwanzo kabisa kule kwenye list ya chaneli nyingi kama picha namba 7 inavyoonyesha hapo juu, kisha utachagua chaneli na utaiadd kama tulivyofanya mfano ktk hii ya ALJAZEERA
- Na kama ukiweza kuendelea na hili zoezi basi utapata chaneli nyingi tu kwa mfano angalia picha namba 11 hapa chini, hii ni FOX NEWS,
- Pia pengine unahitaji kufunga software hii uendelee na shughuli nyingine basi usipate tabu, unachotakiwa kufanya ni kubonyeza mshale huo uliopo hapo chini kulia (kwenye kona) ktk picha hii namba 12, mshale huo umeelekea kushoto,
- Baada ya kubonyeza huo mshale utarudi mwanzoni kabisa ambapo patakuwa panaonekana kama picha namba 14 hapa chini inavyoonyesha,
- Na ukiangalia vizuri picha namba 14 kwa hapo juu, kwa chini kabisa upande wa kushoto mwa hiyo picha kwenye kona utaona kuna button fulani kama ya kuwashia simu au Computer
- Basi kama unahitaji kufunga software yako unatakiwa kubonyeza hapo, na baada tu ya kubonyeza hapo, basi kuna kitu kitatokea kama hiki hapa chini kwenye picha namba 15,
- Ninaamini hapo ktk picha namba 15 umeliona neno “Exit” basi ukilibonyeza tu utakuwa umefunga software yako.
- Angalizo la mwisho kabla sijatoa link hizi mbili, kwa wale wenye simu za mkononi mnaweza kuipata software hii kwa kuingia play store, na kuandika neno Kodi kisha mkasearch mtaiona, na mara nyingi huwa inakuwa ya kwanza kabisa, au ukiona huko ni tabu basi download kwa kutumia link hizi hapa chini;
No comments: