» » Zuia Kuibiwa Vifaa Vya Ndani Vya Computer Yako

Kwanza kabisa unatakiwa ufahamu kuwa sio rahisi kuweza kufahamu kila kifaa cha Computer yako kilicho ndani, lakini hapa ninakuwezesha kufanya hivyo kwa njia nyepesi kabisa.
Leo nimekuletea Software maalum kabisa kwa ajili ya kulist/Kuorodhesha kila kilichomo ndani ya Computer yako, kwa majina pamoja na Model zake, hivyo basi unaweza kuvirekodi pembeni hata ktk Diary yako kwa usalama zaidi, ili ikitokea umetofautiana na fundi wako basi unafungua software yako na kisha unaiomba ikuorodheshee vifaa vya Computer yako na hapo utaweza kucompare kama ni vilevile ulivyovirekodi mwanzo au sivyo, na mwisho kabisa utafahamu ukweli uko wapi.
Uzuri wa software hii ni kwamba;
  1. Haina saizi kubwa (MB 4.9 tu)
  2. Ni rahisi kutumia
  3. Haina kona nyingi wakati wa kuinstall
Zifuatazo ni hatua za kuinstall kisha majibu yote leta Facebook;
  1. Utadownload software hii kwa kupitia link nitakayoitoa hapa chini
  2. Utainstall kama kawaida
  3. Wakati wa kuinstall haitaomba password na ni free kabisa
  4. Ukimaliza kuinstall nenda kwenye desktop kisha itafute utaona imeandikwa “Speccy”
  5. Double click/Ibonyeze mara 2 harakaharaka ili kuifungua
  6. Ikifunguka itakuja kama hivi inavyo onekana hapa chini

Max IT Club speccy

Sasa basi hapo unaweza kuona mwenyewe vitu gani vimeorodheshwa kwa majina, saizi pamoja na modeli zake, kwa mfano;
  1. CPU/PROCESSOR/(UBONGO WA COMPUTER)
  2. RAM/(VITUNZIO VYA DATA KWA MUDA ZINAOTUMIKA)
  3. MOTHERBOARD/(KIFAA KINACHOUNGANISHA VITU VYOTE NDANI YA COMPUTER)
  4. STORAGE/HARD DISK/(KIFAA KINACHOTUNZA DATA ZAKO ZOTE)
  5. N.K
Wengi wetu huibiwa RAMHDDMOTHERBOARD naPROCESSOR, hivyo basi unatakiwa kufahamu vitu vidogo kama hivi ili kuepusha matatizo na mtu, na sio lazima awe fundi tu, wapo hata marafiki wasio waaminifu ambao tunawaazima Computer lakini zinarudi zimebadilishwa vitu.
Sasa basi download Hii software kwa kubonyeza link hii;

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply