» » Je, Unajua Kama Facebook Wanafuatilia Eneo Ulilopo Ili Kupendekeza Marafiki? Jua Jinsi Ya Kujiweka Salama!


Info Post

Image result for facebook trace location
Hivi ulishawahi shangaa katika Facebook, kile kipengele cha “People You May Know” kinaonyesha watu/mtu ambae umetoka tuu kuonana nae hata kwa bahati mbaya?

Ndio! inatokea hii pia, Zamani nlikuwa nafikiri labda inaonyesha watu tuu ambao unaingiliana nao marafiki (Mutual Friends) katika mtandao huo lakini kumbe sio hivyo tuu.

Yaani hapa hapa unaweza ukashangaa kuwa mtu ambae uko nae katika eneo moja
kwa mfano labda uko kwenye mkutano au hata katika tafrija na ukaondoka bila kubadilishana mawasiliano na mtu. Usije ukashangaa unarudi nyumbani na unakuta Facebook inapendekeza uwaongeza watu hao katika listi ya marafiki zako katika mtandao huo.

Unaweza ukashangaa mtandao huo wa kijamii wa Facebook unakuambia hata umu ‘Add’ mtu hata Yule ulietoka kuzinguana nae jana tuu ukiwa bar (Hahah!)
Hii ni hatari sana kwani mtu akiona jina lako na picha yako ana uwezo mkubwa wa kuweza kusoma ‘Profile’ lako kiundani na hata kuweza kujua taarifa zako zingine kama vile unapokaa, unapo soma au hata kazi yako
Hapa Facebook inatumia teknolojia ya eneo (Location) ili kupendekeza uwaongeze watu Fulani katika akaunti yako ya facebook. Usije ukashangaa unapata ombi la urafiki kwa mtu na ukiiangalia sura yake unahisi umeshaiona sehemu lakini hukumbuki ni wapi basi hapo jibu uwe nalo kuwa ni Location
Kwa watumiaji ambao hawahofii mtu kuwafutailia nyendo zao katika mitandao ya kijamii wanaweza wakaendelea kutumia mtandao kama kawaida japokuwa na wenyewe wanatakiwa kuwa na uangalifu mkubwa.
Kwa Wale Ambao Wanahofia Jambo Hili Inawabidi Wafanye Yafuatayo.
Kwa Android: Nenda katika Settings > Apps > Facebook > Permissions > Location – na kisha izime (hii inaweza ikategemea na program endeshaji ya kifaa chako ukiona inashindikana basi unaweza ukazima kabisa ‘Location’ katika kifaa chako)
Kwa iOS: Nenda katika Settings > Privacy > Location Services > Facebook na kisha Chagua ‘Never’ katika machaguo yaliyopo
Ukifanya hivyo hii itaweza kukusaidia katika kuweza kuikata Facebook kutumia taarifa za eneo ulilopo katika kukutumia mapendekezo ya marafiki ambao upo nao katika eneo moja.

Japokuwa Facebook wenyewe wamekataa kuhusiana na jambo hili. Wamesema hawategemei taarifa za mahali ili kuhakikisha kuwa wanawaunganisha watu – kutoa mapendekezo yak u ‘Add’ watu – karibu.

Niambie hii imekaaje? Niandikie hapo chini sehemu ya comment kwani ningependa kusikia kutoka kwako.

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply