Hapa ndio mahali husika katika kujifunza namna ya kuwa na blog yako na kuifanya iwe na mafanikio makubwa kama ambavyo wengine wamefanikiwa kupitia blog zao.
Kuna namna mbali mbali za kuwa na blog ila leo hapa nitazungumzia mbili tu ambazo ni rahisi sana. Kumbuka kuwa kuwa na blog yako mwenyewe hakuna gharama yoyote zaidi ya muda wako na ubunifu wako.
BLOGGER Kupitia uwanja huo au platform hiyo inayomilikiwa na Google unaweza kuanzisha blog yako mwenyewe ambayo itabebwa na jina ulipendalo wewe mfano:- http://blogyako.blogspot.com, hapo ambapo nimekoleza kwa maandishi ya rangi nyekundu ndipo ambapo utaweka jina la blog yako. Utaratibu mzima utaupata wakati ukiwa unaisajiri blog yako Bofya hapa ili kutengeneza blog yako Create a new Blog
WORDPRESS Hapa pia utaratibu ni kama hapo mwanzo ila hizi ni nyanja (Platforms) tofauti na zinatofautiana vikolombwezo (features) vya uboreshaji wa blogs. Hapa ukianzisha blog yako itabebwa na uwanja au platform ya wordpress. Namna ya jina la blog yako itakuwa katika mfano huu:- http://blogyako.wordpress.com. Ukitaka kuwa na blog kupitia wordpress tafadhali bofya hapa, Sign up For New Wordpress Naamini hadi sasa umeisha elewa namna ya kuweza kuanzisha blog yako, wakati mwingine nitazungumzia jinsi ya kuweza kuwa na blog yako ikiwa na domain yako mwenyewe mf:- www.domainyako.com kwa leo nisikuchoshe naishia hapa.
No comments: