» » LINDA POST ZAKO HUKU UKIONGEZA IDADI YA WATEMBELEAJI



Habari zenu ndugu watembeleaji wa blogu hii. Natumaini ni wazima wa afya na karibuni tena katika blogu hii. Leo nawalenga sana mabloga wenzangu na hata kama wewe pia utakuwa na ndoto za kuwa bloga basi hii inakuhusu.

Nimeona baadhi ya blogu zimefungia habari zake ili zisikopiwe na watu wengine ikiwa wao wamezikopy kutoka kwa bloga wengine. Wamezuia "text selection" na pia wameondoa "Lightclick function" lengo lao mtu asikopy habari yake. Kiukweli hii sio njia sahihi hata kidogo nikiwa bloga kama bloga napingana nayo na ni ngumu kuendelea kwa wewe ambaye umefunga habari zako zisikopiwe na bloga wengine.

Miongoni mwa njia nne za kuzuia mtu asikopy habari zako na kuziweka kwake zipo pia hizo za kuzuia "text selection" na "Remove rightclick funtion" Lakini kwa ulimwengu wa sasa sio nzuri sana kwani itakupotezea number of visitors katika blogu yako

Njia hizi hapa ndiyo nzuri sana kwa ulimwengu wa sasa njia hizo ni;

Water mark
DMCA
1.WATER MARK
Kiukweli kabisa njia hizi wewe kama bloga ndio njia nzuri za kuzitumia karne hii ya 21.Water mark inakusaidia kuongeza namba ya visitors yaani watembeleaji katika blogu yako au website.Hii watermark inawekwa katika picha za habari unazoziweka.Mfano mzuri tazama picha za "Millardayo "na " Global publisher" Hawa wanatumia water mark katika picha zao




.
Hiyo ni watermark ya Millardayo.com ambayo itamfanya apate watembeleaji wa kutosha katika website yake kwa yeyote atakaye ikopy ina kuwa ni rahisi kujua kwamba ameikopy kutoka kwa millard ayo hivyo siku nyingine ataenda moja kwa moja kwa millard lakini chanzo ni wewe kukopy habari yake.

Mfano mwingine huu hapa kutoka global publisher


Hiyo hapo ni water mark ya Global publisher ambayo itawatambulisha kwa yeyote atakaye kopy.


2.DMCA
Hapa katika DMCA Itakusaidia kukuongezea idadi ya page view kwa yeyote atakaye kopy habari yako. DMCA Hili ni kampuni la kuzuia duplicated content katika search engine kama google na nyinginezo.Kama wewe ni mvivu wa kuweka water mark basi tumia njia hii itakusaidia kwani Ukisha jiunga na huduma hii wao DMCA Watapokea message kutoka kwako kupitia e-mail yako.Ile habari yako ambayo imekopiwa, yule aliyekopy atapelekewa ujumbe kwamba search engine imegundua kuwa hii habari umeikopy kwa hiyo watembeleaji watakaoifungua katika blogu ya yule aliyekopy itaongeza page view kwako kawani inahesabika kama ya kwako.Mfano mzuri Blogu ya MALUNDE 1 BLOG Anatumia hii.
Kwa leo naomba tuishie hapa kama ukihitaji maelezo zaidi kuhusu DMCA Wasiliana nami kwa namba iliyopo katika bunner hapo juu kabisa mwanzoni 

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply