» » Kujinasua Kwa Wanaotumia Account Yako Ya Facebook


Habari Yako Mpendwa mpenda kufahamu ujuzi juu ya teknolojia,
Hapa nakuletea Mbinu Nyepesi itakayokusaidia kutambua kama Account Yako ya facebook ipo katika hali zifuatazo;
  1. Kama kuna mtu anaitumia bila wewe kujua
  2. Kama ulilog in kupitia Computer au Simu nyingine ukasahau kulog out na unawasiwasi kuna mtu anafuatilia mambo yako
Pia hapa chini nitakufundisha namna ya kujinasua ktk hali hizo hapo juu,
Hatua za kufuata ili kutambua mambo hayo;
  1. Log in ktk account yako ya facebook
  2. Ukiwa katika timeline yako, yaani page yako mwenyewe ambapo unaona cover page yako, angalia katika hiyo Cover page upande wa kulia kwa chini utaona button imeandikwa (View Activity Log) na hapo hapo kwenye hiyo button kwa kulia kwake utaona vidoti vitatu (…)
  3. Shida yetu ni vidoti vitatu na si kingine, na kama umeviona basi naomba tuendelee
  4. Bonyeza hivyo vidoti vitatu
  5. Utaona kuna option 3 zimetokea
  6. Inayotuhusu ni option namba mbili iliyoandikwa (Timeline Settings)
  7. Basi kama umeiona ibonyeze
  8. Itakupeleka moja kwa moja kwenye page nyingine
  9. Ukiwa hapo angalia kushoto juu utaona Option namba mbili imeandikwa (Security)
  10. Basi ibonyeze hiyo option iliyoandikwa Security
  11. Utaona option nyingine nyingi zimefunguka na inayotuhusu ni moja tu
  12. Ktk hizo option zilizofunguka, angalia kutokea chini utaona option kama ya tatu kutoka chini imeandikwa (Where You’re logged in)
  13. Basi kama umeiona ibonyeze
  14. Baada ya kuibonyeza itakulistia kila kitu yaani kwa maana nyingine itakufungulia sehemu zote ambazo account yako ya facebook ipo wazi na inaonyesha hadi jina la kifaa kinachotumika kama ni simu au Computer
  15. Sasa basi, kwenye kila option utaona sehemu imeandikwa(End Activity)
  16. Kazi kwako kuzizimisha activity zote ambazo huzitambui kwa kubonyeza hiyo sehemu iliyoandikwa (End Activity)
Kuna mengi mazuri yanakuja kaa karibu nami tuyajenge

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply