Tecno P5 ni smartphone kutoka china na huwa zipo kwenye kundi moja linalo julikana kama mtk device. Natumaini wapo watu wengi sana wanaotumia Tecno P5 na baadhi ya watumiaji wa simu hizo hupata matatizo kama simu kutowaka au haisomi network au inazima na kujiwasha yenyewe.
Matatizo yapo mengi sana na zipo njia mbali mbali ambazo mtumiaji anaweza kutumia ili kuiponyesha simu yake.
Leo tutaona jinsi ya kuiponyesha Tecno P5 ambayo haiwaki, au inawaka lakini inaishia kwenye neno Tecno au haisomi network. Tatizo la kutokuwaka inawezekana simu ikawa ina matatizo kwenye hardware au software. Mimi nitazungumzia kwenye upande wa software. Maelekezo nitakayo yatoa yatakusaidia kuirudisha Tecno P5 kama ilivyokuwa mpya wakati unaitoa kwenye box
JINSI YA KUIFUFUA AU KUIPONYESHA TECNO P5 AMBAYO HAIWAKI
VIGEZO NA MASHARTI.
1: MIMI SITAHUSIKA KWA CHOCHOTE KILE KITAKACHO TOKEA
2: UELEWA WA COMPUTER UNA HITAJIKA (muhimu)
3: SOMA MAELEKEZO KWA UMAKIMI KABLA UJAJARIBI KWENYE SIMU YAKO
STEP 0
Hakikisha kwenye computer yako tayari ume install google usb driver. Kama bado tembelea link chini
STEP 1
Hakikisha kwenye computer yako tayari ume install vcom mtk drivers. Kama bado tembelea link chini kujua jinsi ya kuweka vcom drivers kwenye computer yako
STEP 2
Download Sp flash tool kwa kutumia link chini kisha extract hilo file kwenye computer yako na utapata muonekano kama picha chini
STEP 3
Download Tecno P5 stock rom kwa kutumia link chini kisha extract hilo file kwenye computer yako na utapata muonekano kama picha chini
STEP 4
Fungua folder la sp flash tool ambalo limepatikana kwenye step 2 kisha run as administrator program inayoitwa flash_tool kama picha inavyoonyesha chini
STEP 5
Baada ya sp flash kufunguka utapata muonekano kama picha chini. click sehemu iliyoandikwa scatter loading.
STEP 6
Computer itakwambia uchague scatter file lako. Scatter file lipo kwenye folder ambalo ulilipata baada ya ku-extract file ambalo uli download kwenye step 3. Jina la folder ni File_to_flash kisha utaona file ambalo limeandikwa MT6572_Android_scatter kama picha inavyo onekana chini. Chagua hilo file kisha chini kabisa bonyeza open
STEP 7
Endapo utafanikiwa basi utapata muonekano kama picha chini. Kama bado ujapata muonekano kama wa picha chini tafadhali rudia tena step zote
STEP 8
Bonyeza kipengele kilicho andikwa download kama picha inavyo onekana chini
STEP 9
Toa battery kwenye simu yako ya Tecno p5 kisha chomeka usb cable kwenye Tecno P5 kisha chomeka kwenye computer yako kisha subiri kama dakika 10 maximum. Endapo utafanikiwa utaona screen inayofanana na picha chini.
Note
Kama ujapata muonekano kama huo hapo juu hakikisha unarudia tena step 0 na step 1 kwa umakini.
STEP 10
Rudishia battery kwenye simu yako ya Tecno kisha washa simu yako.
No comments: