» » SAMSUNG GALAXY NOTE 7/ TCRA YAPIGA MALUFUKU YA UUZAJI WA SAMSUNG GALAXY NOTE 7 TANZANIA

Samsung Galaxy note 7/ TCRA Yapiga malufuku ya uuzaji wa Samsung Galaxy note 7hapa Nchini,,,
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
imepiga marufuku uingizaji na usambazaji wa
simu za mkononi za Smartphone Samsung
Galaxy note 7 kwa kuwa zina matatizo ya betri.
TCRA pia imewataka wananchi ambao tayari
wanatumia simu hizo kuzizima na kuzirudisha
haraka katika maduka walikozinunua.
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy,
amewataka watanzania wajihadhari kuitumia
simu hiyo kwa kuwa Kampuni ya Samsung
yenyewe imeiondoa sokoni.
“Simu hiyo tayari Samsung wenyewe wamesema
ina matatizo ya betri na mara mbili sasa
imelipuka,” amesema Mungy.
Amewaomba watu wenye simu za aina hiyo
kuzirudisha madukani haraka wabadilishiwe ama
kurudishiwa fedha zao.
“Hata kama uliletewa zawadi kutoka nje ya nchi
nawaomba warudishe huko kuepuka matatizo
yanayoweza kujitokeza,” amesema Mungy.
Hivi karibuni simu aina hiyo iliyothibitishwa na
kampuni hiyo kuwa ilikuwa salama, ilishika moto
kwenye ndege nchini Marekani.
Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa
mikononi mwa abiria aliyekuwa kwenye shirika la
ndege la Southwest Airlines.
Shirika hilo liliwaondoa kwa dharura abiria
waliokuwa kwenye ndege iliyokuwa imepangiwa
kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi
Baltimore, Maryland muda mfupi kabla ya
kupaa.

About Unknown

Hi there! I am Hung Duy and I am a true enthusiast in the areas of SEO and web design. In my personal life I spend time on photography, mountain climbing, snorkeling and dirt bike riding.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

1 comments:

  1. Samsung Galaxy Note 7/ Tcra Yapiga Malufuku Ya Uuzaji Wa Samsung Galaxy Note 7 Tanzania >>>>> Download Now

    >>>>> Download Full

    Samsung Galaxy Note 7/ Tcra Yapiga Malufuku Ya Uuzaji Wa Samsung Galaxy Note 7 Tanzania >>>>> Download LINK

    >>>>> Download Now

    Samsung Galaxy Note 7/ Tcra Yapiga Malufuku Ya Uuzaji Wa Samsung Galaxy Note 7 Tanzania >>>>> Download Full

    >>>>> Download LINK EP

    ReplyDelete